Tiganya vincent na Ingiahedi Mduma, Abidjan
Nchi ya Afrika zimetakiwa kuwa na uchumi huru usiotegemea mataifa yaliendelea ili kuepuka kuathirika kuyumba kwa uchumi kwa mataifa makubwa.
Mkurugenzi wa masuala ya maendeleo ya uchumi kutoka Ushirikiano wa maendeleo Afrika(NEPAD) Profesa Emmanuel Nnadozie alitoa kauli hiyo jana mjini Abidjan wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya funzo ambalo Afrika imelipata kutokana na tikisiko wa uchumi duniani.
Alisema kuwa hatua hiyo inawezekana iwapo nchi za Afrika zitaimarisha uchumi mchango5diversity economy) usiotegemea zao moja kwa ajili ya kuingiza fedha za kigeni.
Profesa Nnadozie aliongeza kuwa pia nchi za Afrika zinapaswa kuhasisha ukuaji na ukusanyaji wa mapato ya ndani kama nchi ya kujitegemea.
Aidha alisisitiza kuwa Serikali za Afrika zinapaswa kuunga mkono kwa dhati juhudi za sekta binfasi ili ziweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi wengi barani humo.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwepo na mabadiliko ya haraka na chanya kwa nchi za Kifrika hali itakayowafanya kuonekana uchumi wa unazidi kuimarika.
Naye Mchumi na mtafiti kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Peter Walkenhorst Serikali za Kiafrika zinapaswa kushirikiana sekta binafsi kuongeza nguvu katika umarisha miundo mbinu kama hatua ya kuimarisha uchumi wao wa ndani.
Alisema hatu hiyo itasaidia kuwekeza zaidi katika miundombinu mbalimbali kama vile barabara, reli, usafiri wa majini na anga.
Aliongeza kuwa kutokana na ushirikishaji sekta binafsi sekta ya mawasiliano ya simu imefanikiwa kupanua kwa kasi kuliko sekta nyingine ambazo bado zinategemea nguvu za serikali ili kuimarishwa.
Katika hatua nyingine Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo anatarajia kufungua Mkutano wa 45 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Alhamis wiki hii , mkutano huo unawajumuisha wajumbe mbalimbali duniani.

0 comments:
Post a Comment