KILELE CHA SIKU YA UTAMADUNI SINGIDA KATIKA PICHA!!

Bi. Hadija Mohamed kutoka kikundi cha ngoma za asili Msake kata ya Madewa mkoani Singida akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika namna wanavyoweza kusaga vitu mbalimbali kwa njia za asili bila kutumia mashine leo wakati wa kilele cha maonyesho ya siku ya Utamaduni duniani inayoadhimishwa kitaifa katika uwanja wa Mandela mkoani Singida.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Wasanii wa vikundi mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika kushiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya Utamaduni ambayo kitaifa ianafanyika mkoani Singida.



Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akipata maelezo kutoka kwa msanii na mchongaji Bi. Mwandale Mwanyekwa (kushoto) kuhusu vifaaa mbalimbali yakiwemo mabegi, mikufufu na bangili za wanawake zinazotengezwa kwa vitu vya asili leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kitaifa katika uwanja wa Mandela mkoani Singida.

Wananchi na wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mkoani Singida wakifuatilia matukio mbalimbali ya utamaduni leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Utamaduni Duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Singida.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment