JESHI LA WANANCHI LAMALIZA UKARABATI WA RELI YA KATI!!


Matukio ya picha mbalimbali za Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) zikimuonyesha Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Abdurahman Shimbo akimpa maelezo katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu wakati wa kukabidhi reli ya kati baada ya ukarabati wa reli hiyo hapo jana kwa Wizara ya Miundombinu iliyoharibiwa na mvua mwishoni mwa mwaka jana (dec 2009) kati ya maeneo ya Gulwe hadi Kilosa mkoani Morogoro. Ukarabati huo wa 68 km umegharimu shilingi 15.6 bilioni (tz) .ambao Jeshi la wananchi limekamilisha agizo la RaisJakaya Kikwete kulitaka kukamilisha ukarabati huo kwa haraka ili wananchi kuondokana na kero ya usafiri pamoja na kuiletea taifa mapato ya uchumi.Kwa wakati huu itaanza kutumika kwa treni za mizigo hadi itakapotangazwa rsami kuanza safari za abiria.Picha zote na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Abdurahman Shimbo akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa wa Wizara ya Miundombinu Eng.Omar Chambo wakikagua darala la Munisagala

Mfanyakaizi wa TRL akiwahi katika kazi zake eneo la Mzaganza Kilosa jana.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Jenerali Abdurahman Shimbo akiongozana na Eng. Omar Chambo (kulia) wakikagua eneo la Mkadage Kilosa


Mafundi wakifanya ukarabati wa reli katika eneo la Kidete

Treni ikipita katika eneo la reli lililochukuliwa na maji mwisho wa mwaka jana (Dec.2009) huko Kilosa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment