Dr. Yeronimo Mlawa ambaye ni afisa mradi wa Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio (Champion) inayohamasisha watu kuzungumza zaidi juu ya mahusiano ya kimapenzi ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi katika jamii katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Coutryard Upanga jijini Dar es salaam.
Afisa huyo amesema utafiti unaonyesha kuwa asilimia 6 ya wanandoa wamepata maambukizi kitu ambacho kinaonyesha kwamba hawazungumzi na wala hawajiandai katika mahusiano ya unyumba kitu ambacho kinapelekea mmoja wao kutoka nje ya ndoa yake na kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya Ukimwi.
Amesema kwamba ni kama vile maadalizi ya chakula yakiwa mabaya maana yake kwamba hakiwezi kuliwa vyema na hakuna atakayefurahia kula chakula kile, lakini kama kikiandaliwa vizuri na kikapikwa vizuri kila mmoja anatamani kukila hivyo hata wandoa watakua chakula chao na kufurahia.
Kampeni hiyo itaendesha kwa kutumia matangazo mbalimbali ya Redio, Televisheni, magazeti na vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali kuhusu mapambano ya ukimwi.
aliyeko pichani kulia ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa mradi wa Champion Lindsay Hugres.
0 comments:
Post a Comment