GARI ZA MIZIGO ZAHARIBIKA OVYO NJIANI

Na mdau Emmanuel Joseph
Kaka pole kwa majukumu na kazi. nataka nikujuze habari za muda si mrefu nilizokutana nazo live muda si mrefu.nilikuwa nikitokea A.town kuja dar.
Niliwasili majira ya saa saba na nusu maeneo ya mto wami na kukuta foleni kubwa mno katika kufanya utafiti na kusogea mbele ya tukio. kulikuwa na gari kubwa la mizigo lilikuwa limeshindwa kupandisha kile kijimlima cha pale wami na kutanda barabara nzima na kusababisha foleni kubwa ya magari yakitafuta njia ya pembezoni mwa barabara ambayo ni hatari kwa tahiri likiteleza kidogo linadondoka.
Kwa mantiki hii tumekaa zaidi ya nusu saa tukibanana kwa njia moja tu.na mpaka naondoka sehemu ya tukio hakuna wananchi au maafisa usalama waliojitokeza kulisukuma hilo gari pembeni ili kuruhusu magari yanayopandisha na kushuka yawe yanapita kama kawaida.pia tukio kama hilo nimelikuta tena hapa karibu na mbezi mwisho alimaarufu kama msikitini.
Nimekumbana na gari la mafuta nalo limekwama kupandisha kijimlima kidogo ambacho unaitafuta mbezi mwisho na kusababisha tela lake kukaa katikati ya barabara na kichwa kutizamana na kusababisha foleni kubwa mno na kuzuia magari yanayotoka jijini na yanayoingia jijini kupita kwa tabu sana na kusababisha uchelewaji wa abiria kufika sehemu husika kwa muda unaotakiwa.dhumuni kubwa langu ni kukuomba uwajuze au uwapashe wahusika na maafisa husika wa barabarani na sehemu husika kufika eneo husika na kutoa msaada wa kuyaondoa magari hayo ili wasafiri na magari yaweze kuendelea na safari zao.
Pia wakumbushe maafisa wa usalama barabani wawe wanafanya doria sehemu zao husika hasa za vilimani au kwenye mwinuko.nimeambatanisha baadhi ya picha ya sehemu husika.asante.nawakilishamimi mdau wako

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment