DARAJA LA UMOJA NI ZAIDI YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI!!


Na Joseph IshengomaMAELEZO, MTWARA.

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Emilio Armando Gebuza wa Jamhuri ya Msumbiji leo (tarehe 12/5/2010) wamewaongoza mamia ya wananchi wa nchi zao katika kuzindua daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji.

Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwa nyakati tofauti katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara na Negomano katika jimbo la Cabo Delgado Msumbiji na kuhudhuliwa na Maaris wastaafu wa Tanzaniai Mzee Ali Hasani Mwinyi na Benjamin Mkapa, Rais Kikwete amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi w nchi hizo mbili.“Tumejinyima kutumia fedha za walipakodi wetu wa nchi zetu mbili.

Darja hili ni muhimu kwa wakazi wa nchi hizi mbili na kichocheo kitakachobadilisha kwa kasi maisha ya wakazi wa Msumbiji na Tanzania, “ amesema.“Haikuwa rais kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hili.

Wakati nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, niliwahi kutumwa na RAis Benjamin Mkapa kwenda Japan kuomba ufadhili wa daraja hili. Nilipowaeleza waliniambia kuwa hawawezi kutoa fedha kwa ujenzi wa daraja linalotoka kusikojulikana kwenda kusikojulikana,” ameueleza umati uliokuw aukimsikiliza katika eneo la Mtambaswala.Kwa mujibu wa Mhe Kikwete, baada ya kukosa ufadhili, Marais wa staafu wan chi hizo mbili Benjamin Mkapa na Joachim Chisano wa Msumbiji waliamua kutumia fedha za nadni kulijenga. “Baada ya kushindwa kupata wafadhili marais hawa walitoa uamuzi wa kijasiri kujenga daraja kw akutumia fedha za nadani mbali na nchi ihizi kuwa maskini,” amesema.

Aidha ameeleza kuwa uamuzi wa ujenzi wa daraja hilo lililotumia shilingi bilioni 37.15 ni moja kati ya kazi muhimu zilizotaka kufanywa na waasisi wan chi hizi mbili (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Samora Machel) walitaka kufanya lakini hawakubahatika kufanya.

Aidha Rais Kikwete ameagiza Idara ya Uhamiaji na jeshi la polisi nchini ikuhakikisha wanafungua vituo vyao mapema iwezekanavyo ili kutoa huduma kwa watumiaji wa darja hilo.
“Isije ikafika miezi mitatu kabla hamjafungua kituo hapa.

Nawaomba wahusika waharakishe ujenzi wa kituo hiki ili watumiaji wa daraja hili wanufaike na huduma ya ushirikiano wa taasisi husika bila usumbufu.”Kwa upande wake Rais Gebuza amelesema kuwa ufunguzi huo wa daraja la Umoja utafungua milango ya uwekezaji na kuinua kipato cha wakazi wa pande zote mbili.“Wawekezaji wa miradi mbalimbali watakuja kubadilisha eneo hili na tayari kuna miradi tunayoona hapa iliyoanza baada ya kukamilika kwa daraja” amesema na kuongeza kuwa hii ni ishara kuwa nchi hizi mbili zinauwezo wa kupambana na vikwazo zinavyokumbana navyo.

Katika hatua nyingine, Marais hao kwa pamoja wameahidi kufanya kila linalowezekana kujenga barabara inayounganisha nchi hizo katika pande mbili (Mangaka –Mtambaswala Tanzania yenye urefu wa kilometa 65 na Negomano – Muheda kilometa 175) kwa kiwango cha lami katika muda mfupi ujao.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mangoka wilayani Nanyumbu Bwana Jafari Mtando ameeleza kuwa ujenzi wa daraha hilo ni utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na kupunguza gharama za usafiri.“Ilikuwa gharama kubwa kusafirisha mazao ya biashara kutoka msumbiji. Sikufikilia kama tatizo hili lingetatuliwa na serikali za nchi hizi mbili kwa kipindi kifupi. Tulikwisha ona kuw akauli za viongozi wetu kulijenga daraja kama wimbo usiokwisha,” amesema.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment