Kushoto ni Bw.Fred Mpendazoe akizungumza na waandishi wa habari juu ya usajili wa Chama cha Jamii (CCJ) unaotarajiwa kufanyika kesho mapema katika ofisi za Usajili wa Vyama jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu.
Uongozi wa chama cha Jamii Tanzania (CCJ) wamekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa habari MAELEZO leo ili kutangaza rasmi maombi ya usajili wa kudumu baada ya kukamilisha baadhi ya masharti waliyopewa ili wapate usajili huo.
Uongozi wa chama cha Jamii Tanzania (CCJ) wamekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa habari MAELEZO leo ili kutangaza rasmi maombi ya usajili wa kudumu baada ya kukamilisha baadhi ya masharti waliyopewa ili wapate usajili huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa (CCJ) Bw.Richard Kiabo amesema mchakato wa kukiandisha chama cha Jamii ili kupata usajili wa kudumu kama chama cha kudumu hapa nchini Tanzania umekamilika na hivyo amesema maswali ya kuwa (CCJ) kimekufa kutokana na ukimya wa muda mrefu Bw.Kiabo ametumia methali isemayo “Kimya Kingi huja na Kishindo” kwa hiyo chama cha CCJ kilikuwa kikikamilisha baadhi ya masharti ili kiweze kupata usajili huo.
Aidha mwenyekiti wa CCJ Bw.Kiabo amesema wameshituliwa sana na matukio yanayotokea hivi sasa kwa wanachama Viongozi wa Chama hicho katika mkoa wa Mara na Mwanza kwa kukamatwa na kusingiziwa hujuma zisizo na ukweli ndani yake.
Kwa upande wake msemaji mkuu wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa Kishapu Bw.Fred Mpendazoe amesema,aliamua kutoka kwenye chama tawala na kwenda Chama cha Jamii (CCJ) kutokana na sera zake na pia hakuangalia wingi wa malipo ambayo angepewa bali aliangalia chama chenye sera ya kuisaidia jamii.
Bw.Mpendazoe amesema CCJ nitumaini la wafanyakazi na wananchi wanaoishi katika mazingira magumu hivyo tumejipanga kutoa mgombea kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya rais na kinaamini kitafanikiwa tena kwa kishindo kwani watu wankubali sera zake.
0 comments:
Post a Comment