Brazil yamwacha Ronaldinho


Mcheza soka bora wa mwaka duniani mara mbili Ronaldinho ameachwa katika kikosi cha Brazil kitakachocheza Kombe la Dunia.

Tofauti na makocha wa timu nyingine wanaochagua wachezaji 30 wa awali kabla ya mchujo wa mwisho wa wachezaji 23, kocha Dunga tayari ametangaza kikosi cha wachezaji 23, huku wengine saba wa akiba wakiwa wanasubiri iwapo watahitajika au la.

Hii ina maana kuitwa kwa Ronaldinho au mwenzake Adriano kutategemea kama kutatokea mchezaji atajeruhiwa katika kikosi cha awali.

Ronaldinho mara ya mwisho amechezea Brazil mwezi wa Aprili 2009, lakini kutokana na kuonekana kupanda kwa kiwango chake akiwa na AC Milan kulikuwa na matumaini ya kuitwa tena katika timu ya taifa.

Mlinda mlango wa Tottenham Heurelho Gomes ndiye mchezaji pekee katika kikosi cha Brazil anayecheza soka England.

Wachezaji wengine walio katika kikosi cha Brazil waliowahi kucheza soka England ni pamoja na kiungo wa zamani wa Arsenal Gilberto Silva na Julio Baptista, mchezaji wa zamani wa Manchester United Kleberson, na mshambuliaji wa Manchester City Robinho, ambaye kwa sasa anachezea Santos kwa mkopo wa miezi sita ulioanzia mwezi wa Januari.

Brazil, wanaowania kunyakua Kombe la Dunia kwa mara ya sita, imo katika kundi H pamoja na Ivory Coast, Ureno na Korea Kaskazini.

Kikosi cha Brazil
Walinda Mlango: Julio Cesar (Inter Milan), Doni (AS Roma), Gomes (Tottenham Hotspur)
Walinzi: Maicon (Inter Milan), Daniel Alves (Barcelona), Michel Bastos (Olympique Lyon), Gilberto (Cruzeiro), Lucio (Inter Milan), Juan (AS Roma), Luisao (Benfica), Thiago Silva (AC Milan)

Wachezaji wa Kiungo: Gilberto Silva (Panathinaikos), Felipe Melo (Fiorentina), Ramires (Benfica), Elano (Galatasaray), Kaka (Real Madrid), Julio Baptista (Roma), Kleberson (Flamengo), Josue (VfL Wolfsburg).

Washambuliaji: Robinho (Santos), Luis Fabiano (Sevilla), Nilmar (Villarreal), Grafite (VfL Wolfsburg).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment