AMIN NA BARNABA WA THT KUFANYA MAMBO MAKUBWA RBP MISS DAR INTER COLLEGE MEI 27!!

Msanii wa Muziki wa Bongofleva Amin akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye klabu ya Billicanas leo wakati alipokuwa akizungumzaia onyesho lao litakalofanyika kwenye shindano la RBP Dar Inter College litakalofanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Billicanas.
Amesema yeye pamoja na mwenzake Barnaba wataweza kuwapa burudani ya aina yake mashabiki wa urembo wa jiji la Dar es salaam watakaohudhuria katika shindano hilo ambalo utakuwa ni uwakilishi wake wa kwanza wa kitongoji cha Dar Inter College kufanyika kwa mwaka huu baada ya kuundwa rasmi mwaka huu.
Jumla ya warembo 16 wanatarajiwa kuchuana katika shindano hilo linarotarajiwa kuwa la kuvutia kutokana na warembo watakaoshiriki kuwa katika viwango vya ushindani ambapo washindi watatu watakwenda kushiriki katika shindano la Miss Highlearning.
Warembo hao wananolewa na Miss Vodacom Tanzania namba mbili 2009 Beatrce Shelukindo huku Dansa wa siku nyingi Richard Yalomba aka "Bob Rich" akiwapa mazoezi makali ya kucheza kwa ajili ya Shoo ya ufunguzi kwa siku hiyo ya shindano.
Mratibu wa shindano hilo Silas Michel amewataja warembo wanaoshiriki katika shindano hilo kuwa ni Agness Francis, Sanza Mukajanga, Rosemary Muhoza, Pilly Hashim, Rahma Sway, Shone Mwanyanje, Basilisa Biseko, Catherine George, Rose John, Mary Lidya na Cassian Milinga.
Shindano hilo linadhaminiwa na RBP Oil & Industrial technology Ltd, Kmapuni ya bia TBL kupitia bia ya Redds Original Vodacom Tanzania, Shear Illusion, Michuziblog, Janejohn5blog, Fullshangweblog, Mtaa kwa Mtaablog, Condy Bureau Change na Dotnata Decorations
waliopo kwenye picha kutoka kushoto ni wanamuziki Amin, mratibu wa shindano Silas Michael na mwanamuziki Barnarba.
Meneja Huduma wa kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology (T) Ltd Bw. Ibrahim Khatrush ambao ni wadhamini wakuu wa RBP Miss Dar Inter College akiwa katika mkutano nawaandishi wa habari leo.

Warembo wa RBP Miss Dar Inter College wakiwa katika mazoezi makali kabla ya kupanda jukwaani mei 27 mwaka huu kwenye ukumbi wa Billicanas jijini Dar es salaam

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment