Watu wenye silaha Nigeria wamewateka nyara Wajerumani wawili katika eneo linalozalisha mafuta zaidi kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Watu hao wenye umri wa miaka 45 na 55, walitekwa katika jimbo la Abia.
Utekaji huo ni wa pili kuwakumba wafanyakazi wa kigeni nchini humo katika kipindi cha siku 10 zilizopita.
Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na utekaji nyara huo.
Shirika la habari la AFP limeripoti, mmoja wa watu waliotekwa anafanya kazi Port Harcourt, mji mkuu wa jimbo jirani la Rivers, wakati mwengine anatoka mjini Lagos.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema inachunguza tukio hilo.
Picha hii upande wa kushoto inaonyesha ramani ya jimbo la Abia ambako inadaiwa utekanji nyara huo umetokea
0 comments:
Post a Comment