TBL YAWAANDALIA SEMINA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO!!

Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja akizungumza na waandishi wa habari za michezo waliofika katika semina ya siku moja ya namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam,inayoendelea kufanyika katika hotel ya South Beach resort,Kigamboni leo
Washiriki mbalimbali wakiwa katika semina hiyo.
Kampuni ya Bia Tanzania-TBL imeandaa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari za michezo zaidi ya 50 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Semina hiyo inahusu namna ya kuripoti habari za mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo inawahusisha waandishi wa magazeti, redio,televisheni pamoja na Blogu.
Seminina hiyo inafanyika leo hii Aprili 14, 2010, kwenye Hoteli ya South Beach iliyopo Kigamboni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, semina hiyo inawasaidia waandishi wa habari kupata ujuzi zaidi katika kuripoti mashindano hayo ya Kili Taifa Cup na vile vile kuwa na wigo mpana wa masuala mengine ya soka.
Minja alisema, waandishi katika semina hiyo watapata mafunzo thabiti yatakayoratibiwa na kamati ya ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Semina inapambwa na masuala mbalimbali kama vile mechi ambayo itajenga moyo wa ushindani baina ya vyombo vya habari,” alisema Minja.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesema, TBL imekuwa ikiendesha semina kama hizo tangu ilipoanza kudhamini mashindano hayo ya kimataifa miaka minne iliyopita.
“Huu ni mwaka wa pili mfululizo tangu Bia ya Kilimanjaro ambayo ni moja ya bidhaa ya TBL, idhamini mashindano hayo ambayo yamesaidia kuibua vipaji vipya kutoka ngazi ya chini hadi timu ya taifa na katika klabu mbalimbali za soka ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, huu ni mwaka wa nne kwa TBL kudhamini michuano hiyo,” alisema Kavishe.

Mashindano ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya ‘Kuipeleka soka ya Tanzania Kilele cha Mafanikio’ na yatashirikisha timu 24 zitakazocheza katika vituo sita na michuano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 8, 2010 hadi Mei 15. Fainali za mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam.
Vituo vya mashindano hayo ni Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga.
Udhamini wa mashindano hayo umegharimu Sh milioni 850 na kila timu itapata fedha kwa ajili ya maandalizi, usafiri, malazi na vifaa vya michezo.
Kwa muda mrefu, TBL imekuwa ikijihusisha na soka na daima imekuwa ikifurahia kudhamini katika eneo hilo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.
Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle. Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.
TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa ya Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.
kwa maelezo zaidi wasiliana na:

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. wajameni hii ni noma maana naona waandishi wengine wamelala ama sijui macho yangu, maana wanaona muda unaenda na mtoa mada amalizi ,ili watu wakunje mshiko wao siku ipite,kazi kwelikweli?

Post a Comment