Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam hatimaye imehitimisha michezo yake kwa kishindo baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro katika mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Mdau wa timu ya Simba aliyekuwepo uwanjani hapo wakati wa mchezo huo amesema "Simba ilitawala katika vipindi vyote vya mchezo huo hivyo kuwafanya wachezaji wa mtibwa kutoleta madhara yoyote kwenye lango la timu ya Simba.
Katika mchezo huo mchezaji Mussa Hassan Mgosi amedhihirisha uwezo wake wa kupachika mabao na kujihakikishia ufungaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom msimu huu baada ya kupachika magoli mawili katika mchezo wa leo kati ya magoli manne ambayo Simba imeshinda katika uwanja wa Jamhuri".
Magoli mengine yalifungwa na wachezaji Mohamed Kijuso na Ramadhan Chombo "Redondo" hivyo kuifanya timu ya Simba kuhitimisha ligi hiyo bila kufungwa hata mchezo mmoja, Simba mpaka inamaliza michezo yake yote 22 imeshinda michezo 20 na kutoka sare michezo miwili na katika michezo hiyo imechukua pointi zote sita kutoka kwa watani wao wa jadi timu ya Yanga ambayo jumapili iliyopita ilikandamizwa magoli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment