Marekani yataka mkuu wa tume mpya Nigeria!


Marekani inataka mkuu wa tume ya uchaguzi Nigeria abadilishwe kabla ya uchaguzi mpya wa mwaka 2011 kufanyika.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa ya kujitegemea, Inec, Maurice Iwu ametupiwa lawama za kuhusika na dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.
Waziri mdogo wa Marekani wa masuala ya Afrika Johnnie Carson amesema Bw Iwu hakuwa na uwezo wa kuandaa uchaguzi wenye kuaminika.
Nigeria ni nchi ya tatu kusambaza mafuta kwa wingi nchini Marekani.
Uchaguzi wa 2007 uliosimamiwa na Bw Iwu ulikosolewa vikali kwa kutofuata kanuni kama vile kuiba kura na vitisho kwa wapiga kura.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment