Kundi la Muziki la Jahazi Morden Taarab chini ya Mzee Yusuph, siku ya jumamosi litashuka kwenye ukumbi wa Mashujaa Pub Uliopo Vingunguti ambako kutakuwa na Onyesho la kukata na shoka kuanzia saa mbili Usiku
. Mkurugenzi wa Kampuni ya Mashujaa Entertainment Group, Mamaa Sakina(Cash Lady) alisema kuwa burudani hiyo imeandaliwa maalum baada ya kimya kirefu kilichosababishwa na mwezi wa Kwalezima.
Aidha alisema kuwa katika onyesho hilo waimbaji wote wa kundi Jahazi watakuwapo ikiwa ni pamoja na Bi, Aisha Ramadhani, Mwanne Sekuru, sambamba na kiongozi wa kundi hilo Mzee Yusuph (Mfalme).
“ni wakati mwingine tena ndugu zangu wa Vingunguti, kuendelea kupata raha, nimeamua kuwaleta vijana wa Jahazi kutupa Furaha kutokana na kupokea maombi mengi ya ndugu zangu, yaani wakazi wa Vingunguti, walioniomba niwalete tena kwenye eneo letu siku ya jumamosi, kikubwa mimi ninawakaribisha watu wote, na si kwamba ni onyesho la wakazi wa Vingunguti pekee, bali ni Onyesho la watu wote, nikiwa na maana ni kwa ajili ya vitongoji vyote vinavyopakana na Vingunguti, yaani Buguruni, Kipawa, Tabata, Uwanja wa Ndege,Kiwalani, Lumo, na kwingineko kote bila kubagua, kikubwa ni kufika kujumuika na wana wa Jahazi chini ya Mzee Yusuph Mfame, katika kupata raha” alisema Mamaa sakina
Na kuongeza kwamba siku hiyo kutakuwa na onyesho maalum lililoandaliwa na Mzee Yusuph kwa lengo la kunogesha burudani hiyo kwa mashabiki wote wa kundi hilo la Mipasho.
0 comments:
Post a Comment