Goodluck hakumwona Yar'Adua Nigeria!


Kaimu rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, anasema hakuzungumza na Rais Umaru Yar'Adua kwa karibu miezi mitano.
Bwana Yar'Adua hakuonekana hadharani, tangu aliporudi nyumbani Februari, baada ya kutibiwa Saudi Arabia kwa miezi mitatu.
Akizungumza na BBC, Bwana Jonathan hakueleza kama afya ya rais imetengenea.
Lakini alisema, amezungumza na mke na wasaidizi wa rais.
Kuhusu ghasia zilizotokea Jos, ambako mizozo kati ya Waislamu na Wakristo iliyoanza mwanzo wa mwaka, imeuwa watu kadha, Rais Jonathan, alisema fujo hizo ni za kikabila, siyo kidini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment