Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter atakuwa mpatanishi katika mzozo kati ya shirikisho la soka barani Afrika-CAF na Togo.
CAF iliiwekea Togo marufuku ya kushiriki katika mashindano yake yote kwa muda wa miaka minne. uamuzi huo uliafikiwa baada ya Togo kujiondoa kwenye fainali za mashindano hayo yaliofanyika nchini Angola baada ya maafisa wake wawili kuuwawa wakati basi lao liliposhambuliwa kwa risasi katika eneo la Cabinda.
CAF ilidai serikali ta Togo iliingilia kati masuala ya usimamizi wa soka kwa kuiamuri, kikosi chake kujiuondoa kwenye fainali hizo na kurejea nyumbani. Lakini Togo imepinga hatua hiyo na kulishitaki shirikisho la CAF katika mahakama ya kimataifa ya upatanishi CAS iliyoko nchini Uswizi.
Sasa kesi hiyo imesimamishwa huku rais wa Blatter akijitayarisha kufanya kikao cha upatanishi na pande hizo mbili tarehe 7 mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment