Benki ya EXIM ya China yaipiga jeki Tanzania!!

Waziri wa fedha na uchumi Mustafa mkulo kulia akibadilishana hati na makamu wa rais wa benki ya Exim ya China Zhu Hongjie ikiwa ni makubaliano ya mkopo wa dola milioni 170 za marekani kwa ajili ya uendelezaji wa mkongo wa mawasiliano wa taifa na uendelezaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.


Na Tiganya Vincent-MAELEZO
Benki ya Exim ya China imetiliana saini na Serikali ya Tanzania
makubaliano ya mkopo kwa ajili kusaidia miradi miwili ya maendeleo
hapa nchini.

Makubaliano hayo yalifikiwa leo jijini Dar es salam kati ya Waziri wa
Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo na Makamu wa Rais wa Benki ya Exim Zhu
Hongjie .

Katika mradi wa kwanza Benki hiyo imetoa jumla ya Dola za Kimarekani
milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa mkonga wa Taifa wa mawasiliano
awamu ya pili.

Kwa mujibu wa Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo , mkopo huo
utasaidi kuimarisha mawasiliano ya Teknolojia (ICT) ikiwemo uboreshaji
wa huduma za tovuti na simu.

Alisema kuwa msaada huo utasaidia kuchochoea maendeleo katika sekta
mbalimbali kupitia teknolojia ya mawasilano (ICT) na hivyo kuondoa
umaskini.

Aidha Mkulo alisema kuwa pia EXIM Benki ya China itatoa Dola milioni
70 kwa ajili ya kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

Alisema kuwa hatua hiyo itarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria
na mizigo katika visiwa hivyo.

Mkulo alisema mara baada ya kukamilika kwa uboreshaji wa uwanja huo
wakazi na wanachi wa Zanzibar hawana haja ya kuja Dar es salaam kwa
ajili ya shughuli za usafiri badala yake watatumia uwanja huo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkulo ametoa wito kwa wananchi wa China
kuja kuhudhuria Mkutano wa Dunia wa Biashara utakaofanyika mapema
nchini ili kuja kutafuta fursa za uwekezaji.

Alisema mkutano huo unatarajia kujumuisha zaidi ya watu maarufu 800
kutoka sehemu mbalimbali duniani.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment