Na Mwandishi maalum-Washington DC
Mkurugenzi wa Idara ya Fedha na Masoko ya Mitaji Bw. Viñals José amezionya benki kuwa makini na mikopo ili isije kuhatarisha tena uchumi wa dunia.
José alisema hayo juzi mjini Washington DC wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa anatoa ufafanuzi juu ya hali ya uchumi ilivyo hivi sasa duniani.
Bw. José alieleza kuwa katika ripoti yao hatari ya kuyumba kwa uchumi imeondoka na sera zimeimarika kwa kuweka uchumi kuwa imara na madhubuti zaidi walivyotegemea.
Alisema kuwa katika uchumi wa dunia umeanza kurudi katika hali yake ya kawaida hali iliyosaidia kuondoa viashiria vya hatari na vilevile imesaidia Taasisi za fedha kuwa makini.
José aliongeza kuwa pamoja na kuwa uchumi umeimarika bado kuna mambo muhimu ambayo wanapaswa kuyazingatia kama vile hatari zinazoweza kujitokeza hasa kwenye madeni na kuhakikisha kunakuwa na uangalifu wa hali ya juu na kuyafuatilia.
"Tukiangalia kwenye mifumo ya mabenki, inatia moyo kwani uchumi umeimarika na soko la fedha limeongezeka. Makadirio ya kushuka kwa mabenki yameongezeka kwa $500 billion, kutoka $2.8 trillion mpaka $2.3 trillion, na makadirio ya mbili ya tatu yamegundulika hadi sasa.Zaidi ya hapo uwiano wa mitaji ya mabenki kwa ulaya na Marekani umeimarika, na mabenki yameongeza mitaji na kufurahia pato la muda lililoongezwa".alisisitiza mchumi huyo.
Aliongeza kuwa pamoja na mafanikio haya , mabenki bado yanatakiwa kuwa na mitaji mikubwa ukizingatia kuwa hiyo walinayo ni ile ambayo wamepatiwa na shirika la fedha la kimataifa, hivyo basi hawana budi kujifunga mkanda na kutoridhika kuwa sasa wana mitaji ya kutosha.
José alisema kuwa kwa maana hiyo mabenki yote yajue kuwa yana changamoto kubwa ya kifedha ambayo ni kama takriban $5 trillion hadi kufikia miaka mitatu ijayo.
Aliongeza kuwa pamoja na matokeo hayo, mifumo ya mabenki itatakiwa kuwa na msukomo mkubwa wa kuhakikisha kuwa mikopo yote inalipwa japo kidogo kidogo na kuwepo kwa uwezo wa kukopesha.
Aidha alisema kuwa ni vema kuwa waangalifu katika mikopo ambayo inaweza ikahatarisha uchumi wa dunia sio tu kwa mambo ya fedha za umma bali pia kwa uimara wa fedha zote.
Aliongeza kuwa watunga sera ni lazima waendeleze na wawasiliane katika kupanga mambo ya fedha ili kuondoa matatizo yanayoweza kuathiri mambo ya mtiririko wa fedha.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI MKUU
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI-ya Tanzania akiwa
WASHINGTON DC
21/4/2010
0 comments:
Post a Comment