ZANTEL YAJA NA CHOMOKA NA MKWANJA KWA WAKAZI WA ARUSHA NA KILIMANJARO!!

Meneja Mauzo wa Zantel Tanzania Rweyememu Protace akiongea na waandishi wa habari kuelezea jinsi ya kushiriki promosheni ya Chomoka na Mkwanja.

Zantel jana imezindua promosheni ya CHOMOKA NA MKWANJA maalum kwa wakazi wa Arusha na Kilimanjaro. Promosheni hii itawawezesha wateja wa zantel kupata nafasi ya kujishindia milioni 1 kila wiki kwa muda wa wiki 8.
Mgeni rasmi katika hafla fupi ya uzinduzi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Raymond Mushi aliishukuru Zantel kwa kurahisisha mawasiliano kwa kusambaza mtandao wake maeneo mengi mkoani Arusha. “Mtandao wa Zantel umesambaa hadi maeneo mengi ya mkoa wa Arusha na kama mji unaotegemea utalii kiuchumu umeturahisia mawasiliano ya simu na intaneti baina ya wageni, wafanyabiashara, wafanyakazi na wakazi wa Arusha kwa ujumla.” alisema Bw. Mushi.
Akizungumwa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja Mauzo wa kampuni ya Zantel Bw. Rweyemamu Protace alisema kwamba zawadi katika promosheni hiyo ni pamoja na pesa taslim milioni 1, Simu za Nokia pamoja na vocha za muda wa maongezi wa Tsh 10,000.
“Tutakuwa tukitoa shilingi milioni 1 kila wiki, simu 1 ya Nokia 1203, na vocha za muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila wiki kwa muda wa wiki 8 kwa watakaobahatika kujishindia zawadi hizi” alisema Bw. Rweyemamu.
Meneja huyo ameendelea kusema kwamba Zantel imeamua kuzindua promosheni hiyo ili kuwazawadia wateja wake wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambao wamekuwa wateja wa waaminifu wa kampuni hiyo.
Ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja wa zantel atatakiwa kuweka muda wa maongezi wa Tsh 1,000 au zaidi na kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno MKWANJA kwenda namba 15583. Ujumbe huo utatozwa Tsh 350 pamoja na VAT. Mteja anaweza kutuma SMS nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi za kushinda.
Droo za promosheni hii zitafanyika kila Jumatatu ambapo washindi watapigiwa simu na kuarifiwa kuhusu ushindi wao na hatimaye kupewa zawadi zao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment