NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
JUMLA ya visima 6,048 vimechimbwa na Wakalawa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa(DDCA) katika maeneo mbalimbali nchini tangu ilipoanzishwa. Hayo yalisemwa jana na Ofisa Masoko na Uhusiano wa DDCA Nungu Egwaga katika uwanja wa Mwendapole, wilayani KIbaha, ambapo maadhimisho ya 22 ya wiki ya maji kitaifa yanafanyika. "Kati ya visima hivyo 5,139 vimefanikiwa kutuoa maji kwa asilmia 100", alisema Egwaga.Hata hivyo Egwaga aliongeza kuwa maeneo yenye mchanga ndio mazuri kwa ajili ya visima vya.Maji.Alisema uchimbaji wa visima hufanyika kwa gharama y ash 55,000 hadi 60,000 kulingana na eneo. Akizungumzia kuhusu changamoto wanazokumbana nazo katika huduma hiyo alisema kuwepo kwa kampuni binafsi zaidi ya 70 chini zinazoshughulika na suala hilo, ambazo baadhi yao hazijasajiliwa, na kusasabisha kuounguza bei ya uchimbaji visima au kutoaminika.Egwaga alishuauri kampuni hizo zisajiliwe ili kuepusha matatizo kwa wateja.DDCA ilianzishwa mwaka 1997 chini ya Sheria namba 30 ya mwaka 1997, madhumuni yake ni kutafuta vyanzo vya maji na kuviendeleza kwa gharama nafuu ili kuboresha hupatiknaji wa huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment