Timu ya Taifa Taifa Stars imeshinda kwa magoli sita ambayo yamefungwa katika kipindi cha kwanza na cha pili kupitia wachezaji tofauti tofauti wa timu hiyo katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru kati ya Taifa Stars na Somalia jioni hii katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Magoli hayo yamefungwa na wachezaji John Boko dakika ya 17, Kigi Makasi dakika ya 33 katika kipindi cha kwanza cha mchezo, katika kipindi cha pili Mchezaji Mrisho Ngasa amefunga goli katika dakika ya 55, dakika ya 74 amefunga mchezaji Erasto Nyoni, Muss Hassan Mgosi dakika ya 83 na Canavaro amepigilia msumari wa mwisho dakika ya 87 kwa wasomali hao na kufunga kalamu ya magoli 6-0 dhidi ya Somalia.
Mchezo huu ulikuwa ni wa upande mmoja ambapo timu ya Somalia ilikuwa dhaifu katika muda wote wa mchezo huo na kuwafanya wachezaji wa Taifa Stars kuwageuza kama walivyotaka kitu kilichopelekea kukandamizwa magoli hayo sita.
Kwa matokeo hayo ina maana Timu ya taifa Taifa Stars itakwaana na timu ya taifa ya Rwanda na ikifanikiwa kuifurumusha Rwanda katika michuano hiyo itakuwa imekata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa bingwa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN zitakazofanyika nchini Sudan katika jiji la Khatoum kuanzia januari mwakani, Hongera Kocha Marcio Maximo najua utaondoka moyo wako ukiwa safi na wenye faraja tele.
0 comments:
Post a Comment