. TATIZO la kutokuwepo kwa vifaa vya ukoaji hapa nchini limeendelea kusababisha vifo vingi hasa ajali zinapotokea barabarani ambapo vinapohitajika hukosekana hivyo idadi kubwa ya watu kufa eneo la tukio .Hilo limethibitika jana katika tukio la ajali lililotokea eneo la daraja la kibamba jirani kabisa na Mji wa Kibaha ambapo lori lililokuwa na shehena ya mafuta uzito wa lita 30,000 liliigonga gari aina ya Hiace na kuilalia kwa zaidi ya masaa 5 bila ya kuwepo kwa vifaa vya aina yoyote vya uokoaji.Akizungumza katika eneo la ajali hiyo na waandishi wa habari Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohammed Mpinga alibainisha kuwa tatizo hilo lipo si kwa Jiji la Dar es salaam pekee bali ni la nchi nzima.Alisema serikali kwa sasa ipo katika kuendeleza jitihada zake za uletaji wa kifaa cha uokoaji Break Down ,hata hivyo hajaweka bayana muda wa kuletwa kifaa hicho.Ajali hiyo imehusisha lori hilo lenye namba za usajili T 189 ABD iliyokuwa na trela T 192 ABD iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze na Hiace T615 AJN iliyokuwa ikitokea Kibamba kwenda jijini Dar es salaam .Tukio hilo limetokea majira ya saa 11 alfajiri jana na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 11 ambapo baadhi wametambulika kuwa ni Zainabu Ally ,Shukuru Hussein na Abuu Twaibu,na wengine waliotajwa kwa jina moja ambao ni Seif ambaye ni dereva wa Hiace, Bweto na Mama Peter wote wakiwa wakazi wa kibamba.Katika eneo hilo ajali vilio vilitawala zaidi ya masaa manne kutokana na kila aliyefika eneo hilo kuona hali halisi ya ajali hiyo iliyokuwa ya kusikitisha kwani kila maiti iliyotolewa kwenye Hiace hiyo zilikuwa nyingine zikatika vichwa na kiwiliwili,utumbo nje.Majira ya saa 4.30 ndipo break down lenye namba T 407 BDG na T 548 BDS kutoka kampuni binafsi ya Effco Crane iliyokodishwa kwa ajili ya uokoaji iliwasili eneo hilo na kuanza jitihada za kunyanyua lori na kutoa maiti zilizokuwemo ambazo hata hivyo hazikuweza kufahamika idadi kamili kwani zingine zilisagika midhili ya nyama buchani.Hivyo kuwa kazi ngumu hata kwa Jeshi la polisi kupata idadi kamili ya waliokufa katika ajali hiyo mbaya.Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ilitokea wakati fuso la mchanga ambalo namba zake hazikuweza kupatikana ilipotaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele na ghafla lilipoona gari jingine lilirudi katika sehemu ya awali hivyo lori kutaka kuigonga fuso na hivyo kutoka upande wa pili na kukutana na hiace na kuiburuza na kuzama nayo mtaroni na kusababisha ajali hiyo.Polisi kutoka Dar es salaam waliweza kudhibiti hali ya usalama katika eneo la tukio ,kudhibiti wizi kutotokea,uhamishaji wa mafuta katika lori jingine kwa ajili ya kuepusha kulipa kwa moto kutokana na gari hilo kuwa na mafuta .Hata hivyo polisi imesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao madereva wengi hupelekea matatizo kama hayo kutokea,Dereva wa lori ambaye anadaiwa kusababisha ajali hiyo amekimbia baada ya tukio na hadi sasa hajaweza kupatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Hapa likinyanyuliwa na winchi ili kutoa miili ya marehemu waliokuwemo kwenye gari .
SIJUI TUTAFANYAJE JAMANI MAANA WATANZANIA WANAENDELEA KUTEKETEA KWA AJALI!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment