Rais wa Uefa Michel Platini atawania tena kwa muhula wa pili wakati muhula wake wa kwanza utakapomalizika mwishoni mwa mwaka ujao.
Platini amethibitisha uamuzi wake huo katika mkutano wa mwaka wa baraza kuu la Shirikisho la Soka la Ulaya nchini Israel siku ya Alhamisi.
Platini raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 54 aliyechukua hatamu za uongozi kutoka kwa Lennart Johansson mwaka 2007, anatarajiwa kuwania kiti hicho bila kupingwa wakati uamuzi utakapofanywa mwezi wa Mei mwaka 2011 mjini Paris.
Amewaambia wajumbe wa UEFA mjini Tel Aviv "Ni mtu mwenye furaha, Rais mwenye furaha na ni mwenye furaha pia kufanya kazi nanyi."
"Sina kazi nyingine ya kufanya, kwa hiyo kwa furaha nawatangazia mimi ndie mgombea nikisubiri kuchaguliwa kwa muhula wa pili kuwa Rais wa UEFA."

0 comments:
Post a Comment