NA MAGRETH KINABO – MAELEZO KIBAHA
WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amewataka wananchi kuanza utaratibu wa kuvuna maji ya mvua ili kuweza kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji. Aidha Waziri huyo Kiongozi amewataka wananchi kuacha kutumia maji safi la salama katika shughuli za kuoshea magari na kufyiatua mafotali ya kujengea badala yake wavune maji ya mvua ili kuweza kuyatumia katika shughuli hizo. Ushauri huo ulitolewa jana na Nahodha wakati wa kilele cha maadhimisho ya 22 ya wiki ya maji yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Mwendapole wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni Maji Safi na Salama kwa Afya Bora’“ Ushauri wangu kwa wananchi ni kuacha kutumia maji yaliyyotibiwa kuoshea magari, badala yake wavune maji ya mvua na kuyatumia kuosha magari na kufyiatua matofali ya kujengea,. Tukifanya hivyo tutaongeza uwingi wa rasilimali za maji, “ alisema Nahodha huku akiitaka Wizara ya Maji na Umwagiliaji ianze kuonyesha mfano. Waziri huyo Kiongozi alisema asilimia kulingana na utafiti alioufanya karibu asilimia 80 ya maji ya mvua yanatiririka baharini, hivyo hili si jambo zuri, kwani kiwango cha maji ardhini kinapungua hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo wataalamu wanapaswa kubuni mipango ya kuzuia maji hayo yabaki ardhini kwa kujenga mabwawa. Akitolea mdano wa jiji la Dares Salaam, wilaya za Kibaha na Bagamoyo, ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki.“ Kuna haja ya kutunga sheria ndogondogo ili kila mwenye nyumba aanze kuchimba bwawa ya shimo lenye uwezo wa kuhifadhi maji ya mvua lita 2000 ili maji hayo yatumike wakati wa kiangazi,” alisisitiza. Akizungumzia kuhusu tatizo la maji katika jiji la Dare Salaam, Kibaha na Bagamoyo alisema wizara husika imechimba visima 20 katika awamu ya kwanza kati ya 30 vinavyotakiwa kuchimbwa kwenye wilaya ya Mkuranga maeneo ya Mpera na Kimbiji.
Hatua nyingine za wizara hivyo ni kubadilisha mabomba yaliyochaa ili kuokoa upotevu wa maji na kukarabati vituo vya Ruvu chini na kuweka bomba kubwa hivyo hatua hizo zikikamilika tatizo hilo litakuwa limekwisha. Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka na Maji Safi na Maji Taka(DAWASA), Boniphance Kasiga alisema upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini utaongeza mita za ujazo kutoka 180,000 hadi 270,00 kwa siku unafadahiliwa na Milinnnium Challenge Account - Tanzania (MCC) utagaharimu sh. bilioni 20.

0 comments:
Post a Comment