MTEJA WA ZANTEL ACHOMOKA NA VESPA ZANZIBAR!!


Zantel leo imeendesha droo yake ya pili ya promosheni ya CHOMOKA NA VESPA ambapo Bibi Ramla Said amebahitika kujishindia pikipiki aina ya Vespa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo Afisa Masoko wa Zantel Zanzibar Bw. Ibrahim Attas alimpongeza Bi. Ramla kwa kujishindia Vespa hiyo.

“Hii ni droo ya pili ya promosheni Chomoka na Vespa kwa hiyo bado kuna muda wa wiki 6 na droo 6 zilizobakia na zawadi ambazo bado zinashindaniwa ni pamoja na Vespa 6, Baiskeli 18, Simu za mkononi 18 na vocha 30 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000. Zawadi hizi zitaendelea kutolewa kila wiki ambapo tutakuwa tukitoa Vespa 1 kila wiki, baiskeli za kisasa 3, simu za mkononi zinazotumia mwanga wa jua 3 na vocha 5 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila wiki kwa muda wa wiki 6 zilizobakia,” alisema Bw. Ibrahim

Washindi wengine katika droo ya promosheni hiyo ni pamoja na Bw Haji Silima Msukwa, Bi. Mikidadi Silai Silima na Bw Nassor Haji ambao wamejishindie zawadi za baiskeli za kisasa kila mmoja. Bw Ali Mohd, Bw Fuad Ali Jongo na Bw Rubea Khamis ambao wamejishindia simu za mkononi zinatumia nishati ya jua kila mmoja na Bw Ame Khamis, Bw. Ali Mohd Chumbuni, Bw Juma Ramadhan na Bw. Abdul Othman ambao wamejishindia muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila mmoja.

Afisa Masoko huyo ameendelea kusema kwamba washindi wote wanatakiwa kufika makao makuu ya Zantel Zanzibar ili kuchukua zawadi zao.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja wa Zantel atatakiwa kuweka muda wa maongezi wa Tsh 1,000 au zaidi na kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno VESPA kwenda namba 15583. Ujumbe huo utatozwa Tsh 350 pamoja na VAT. Mteja anaweza kutuma SMS nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi za kushinda.Droo za promosheni hii zitafanyika kila Jumatatu ambapo washindi watapigiwa simu na kutaarifiwa kuhusu ushindi wao na hatimaye kupewa zawadi zao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment