MAGRETH KINABO – MAELEZO KIBAHA.
SERIKALI imewataka wakazi wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuhakikisha wanatumia vizuri mradi wa bwawa la umwagiliaji la Msoga ili kuendeleza na kutekeleza sera ya kilimo kwanza, ikiwa ni hatua ya kuweza kuendesha maisha yao na kukuza uchumi.
Wito huo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Christopher Chiza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo, alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, ikiwa ni mojawapo shughuli za maadhimisho ya 22 ya wiki ya maji inayoendelea kufanyika kitaifa kwenye uwanja wa Mwendapole, Kibaha.“Hakikisheni mnzalisha mazao vizuri kwa kutumia mradi huu , ambao gharamza za uwekaji wa miundombinu zimetumia fedha nyingi, alisema Naibu Waziri Chiza.Aidha Chiza aliwata wataalamu wa kilimo cha umwagilaji wanatoa elimu kwa wakulima ili maji ya bwawa hilo yaweze kutumika kwa utalaamu. Katika kusisitizi suala hilo alisema elimu ya shamba darasa itolewe, pia kwa wale wakulima waliopata elimu Mkindo wafundishe wenzao.“Wataalamu wa umwagiliaji hakikisheni maji haya yanatumika vizuri ni lazima elimu ya umwagilijai itolewe kwa wakulima ili wawweze kufahamu ni wakati wa kumwagilia na kulima mpunga,” alisisitiza Waziri. Alizitka kamati za maendeleo ya kata kusimmmia matumizi ya maji kwa wakulima na wafugaji ili kuepusha migongano.
Naibu Waziri huyo, aliagiza pia utafiti ufanyike na matokeo yake yatpatikane ili shughuli za maji na kilimo ziwe endelevu.Awali Kaimu Mkurugenzi waHalimshauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Fidedelica Myovella, ambaye ni Ofisa Kilimo, mifugo na Ushirika alisema wa mradi huo ambao utagharimu sh. bilioni 2.8, unahusisha ujenzi wa bwawa na birika la kunyweshea mifugo ambalo litagharimu sh. bilioni1.9, ambapo ni awamu ya kwanza .
Alisema awamu ya pili ni ujenzi wa miundombinu ya umwagliaji itakayogharimu sh. milioni 879, ambao unahekta 150 utawanufaisha wakulima 200 katikakilimo cha mbogamboga mfano za majani ambazo ni nyanya, bamia, matikiti maji, matngo, pilipili hoho, kabichi, mahindi na mpunga wakati wa masika. Myovella aliongeza kuwa mradi huo, bado unahaitaji sh. bilioni 1.4 iliuweze kukamilika kama ulivyopangwa. Pia unahitaji sh. milioni 105 ikiwa ni ombi maalum kwa ajili ya uchimbaji wa kisima kirefu na mitambo ya uzalishaji maji kutoka chini ardhi ili kuweza kutosheleza mahitaji ya maji katika eneo hilo. Alisema kiasi cha fedha cha sh. miloni 527.9 kinadiwa na mkandarsi wa ujenzi huo ambaye ni SUMA JKT.
Akizungumzia kuhusu fedha hizo, Chiza alisema fedha hizo zitafutwa.Mradi huo umejengwa kupitia fedha zilizotolewa na Mfuko wa Msaada wa chakula wa Serikali ya Japan(FACF) NA Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaj wa Wilaya(DIDF),.
0 comments:
Post a Comment