Rais Kikwete atoa heshima za mwisho kwa Rajabu Kianda aliyekuwa Mnikulu!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa mnikulu Bwana Rajabu Kianda aliyefariki jana jijini Dar es Salaam.Marehemu Kianda anatarajiwa kuzikwa kesho(tarehe 9/2/2010) nyumbani kwao Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Khadija Kianda ambaye ni mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa Mnikulu ambaye alifariki dunia Jumapili jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuifariji familia ya marehemu ambaye anatarajia kuzikwa huko Kihurio Same,Mkoani Kilimanjaro.Pembeni ni Mama wa Marehemu Mwanahawa Samuel.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Bi.Khadija Kianda mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu kufuatia kifo chake kilichotokea jumapili jijini Dar es Salaam.

(Picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Jamani kido hili neno MNIKILU maanayake nini?

  2. Mnikulu au Comptroller kwa kiingereza....Maana yake ni mtu anayeshughulika na mambo yote yanayohusinia na affairs za raisi pamoja na wageni wote wa raisi wanaofikia ikulu.Ndio mtu anayeshughulika na ikulu zote za Tanzania kwa kuhakikisha affairs za raisi zinakwenda vizuri

Post a Comment