Rais Kikwete alipokagua athari za mafuriko kilosa!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda kiberenge tayari kukagua uharibifu wa reliya kilosa Dodoma uliofanywa na mafuriko kando ya mto Mkondoa huko Kilosa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji watoto ambao makazi yao yameharibiwa vibaya na mafuriko ya mto Mkondoa ulioharibu mji wa Kilosa hivi karibuni.

Sehemu ya soko kuu la mji wa Kilosa iliyoharibiwa vibaya na mafuriko yaliyotokana na mto Mkondoa unaopita katikati ya mji huo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kingo za mto mkondoa uliofurika na kuleta hasara kubwa ya mali katika mji wa Kilosa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia reli iliyosombwa na maji ya mto Mkondoa wilayani Kilosa jana(picha na Freddy Maro)




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment