VILIO na simanzi vilitawala leo katika viwanja vya Mahakama ya Rufani baada ya Msajili wa Mahakama hiyo, Jaji Neema Chusi kutangaza kuwaachia huru watoto wa mwanamuzi nguli, Nguza Viking 'Babu Seya' kwa kile kilichosemwa kuwa walifungwa kimakosa.
Hukumu hiyo imeanza kusomwa leo saa 3 asubuhi, ambapo umati mkubwa wa wanamuziki kutoka bendi mbalimbali ndugu na jamaa wakifurika kufuatilia hukumu hiyo iliyokuwa ikisomwa kwa umakini mkubwa.
Naibu Msajili wa mahakama kuu Jaji Neema Chusi alianza kwa kuchambua kosa moja baada ya lingine walilokuwa wanakabiliana nalo wafungwa hao.
Katika mashitaka ya kubaka Jaji Chusi alisema kuwa, jopo lililokuwa likisikiliza rufani hiyo limebaini kuwa, katika mashitaka 10 ya kubaka yaliyokuwa yakiwakabili wafungwa hao Francis Nguza na ndugu yake Johnson Nguza mbango hawakuhusika nalo.
0 comments:
Post a Comment