Mgeni Rasmi Wziri wa Muunganio Mohamed Seif Khatib kulia na Mwenyekiti wa Serengeti Breweriers Jaji Marck Bomani wakiingia katika tafrija ya chakula cha jioni kwa waandishi wa habari kilichoandaliwa na kampuni ya Serengeti Breweriers katika kutambua mchango wa vyombo vya habari na kushukuru kwa ushirikiano wao kwa mwaka uliopita 2009 na kuukaribisha mwqaka mpya wa 2010 iliyofanyika kwenye ukumbi wa makuti Msasani Beach Club jijini Dar es salaam jana, pamoja na kutambua vyomba mbalimbali vya habari zikiwemo televisheni, Magazeti na Redio , pia Serengeti wamefanya kitu kikubwa sana kwa kutambua mchango wa blog mbalimbali hapa nchini ambacho binafsi kama mwanablog siwezi kukisahau na inanipa nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii nawashukuru sana Serengeti kwa kutambua angalau hiki kidogo najua huu ni mwanzo makubwa zaidi yatakuja kadiri tunavyoshirikiana katika kazi mbalimabali.
Mgeni Rasmi katika chakula cha jioni kwa waandishi wa habari kilichoandaliwa na kampuni ya Serengeti Waziri wa Muungano Mohamed Seif Khatib katikati akikata keki ya kuukaribisha mwaka 2010 kwa pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Serengeti Jaji Marck Bomani kushoto na Mhariri mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda na mwisho ni Meneja uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda tafrija hiyo ilifanyika ukumbi wa makuti Msasani Beacha Club jana jioni.
Wazee wa kublog wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Serengeti katika kuutambua mchango wa blog katika kupasha habari, Serengeti wameonyesha njia na wamefanya kitu kizuri sana kwani hii inatupa moyo sana sisi wanablog ili kuendelea mbele na kazi yetu ya kupasha habari umma, katika picha kuanzia kushoto ni John Bukuku wa Fullshangwe.blog, Issa Michuzi wa Issamichuzi.blog,Jofrey Mwakibete wa Mohammeddewji.com/blog, Muhidin Sufiani wa Sufianimafoto.blog na Michuzijunior wa Jiachie. Blog.
Mzee wa Fullshangwe.blogsopt.com John Bukuku kushoto kati ni Mzee wa kujiachia Michuzijunior, Sufianimafoto.blogspot.com Muhudin Sufiani wakicheza muziki pamoja hii ilikuwa ni shangwe na furaha kwao mara baada ya kampuni ya Serengeti kutambua mchango wao na kuwakabidhi vyeti katika sherehe hiyo.
Waziri Seif Maohamed Khatib ambaye alikuwa mgeni rasmi katika chakula cha jioni kwa waandishi wa habari akifungua muziki na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Serengeti Teddy Mapunda.
Hapa wanahabari wakiserebuka kwa kwenda mbele yaani ilikuwa ni kushangweka tu na mambo ya Serengeti.
0 comments:
Post a Comment