Gordon Brown atubu kwa niaba ya Uingereza!


Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown anatarajiwa kuomba msamaha rasmi kwa namna Uingereza ilivyo warejesha watoto zaidi ya laki moja katika koloni zao za zamani.
Hatua hiyo ya Uingereza ilichukuliwa chini ya mpango wenye utata wa kuwarejesha makwao wahamiaji miaka arobaini iliyopita.
Watoto wengi walichukuliwa kutoka kwa familia zao kwa nguvu na kupelekwa nchini Australia, Canada na nchi nyingine za Jumuiya ya madola.
Inasemekana badala ya watoto hao kupata maisha bora, waliteswa kwenye makao ya kuwatunza na walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwenye mashamba.
Waathiriwa sitini wamerejea mjini London kushuhudia Waziri Mkuu Brown akiomba msamaha huo.
Mwezi Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu wa Australia, Kevin Rudd, pia aliomba msamaha kwa waathiriwa hao waliojulikana kama raia wa Australia waliosahaulika.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Wewe Kif wewe! Hivi bado ujui kwamba hii nchi ilishauzwa?

  2. Idadi ya wafanyakazi wa TAKURU haifika hata 900 nchi nzima, hivyo wananchi kudhani kwamba kazi ya kuwafichua wala rushwa itafanya na TAKURU peke yao ni makosa makubwa.

Post a Comment