Ziara ya Makamu wa Rais Dk. Ally Mohamed Shein Wilayani Kilosa!!

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akitoka kukagua moja kati ya mahema ambayo yatatumika kama makazi ya muda kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa katika eneo la Kimamba alipotembelea Wilaya hiyo jana kuangalia kiwango cha athari na misaada inayohitajika.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo ya ujenzi wa makaazi ya muda toka kwa Mkuu wa wilaya ya kilosa Halima Dendegu katika eneo la Magomeni mjini Kilosa jana wakati Dk shein alipofanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko ambayo yameikumba wilaya ya Kilosa kutokana na mto Mkondoa kujaa maji ya mvua na kina chake kupungua.
(Picha na Clarence Nanyaro wa Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiwafariji baadhi ya waathirika wa Mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa wakati alipowatembelea katika eneo la Magomeni jana ambako inajengwa kambi ya muda ya kuwasitiri wananchi hao ambao kwa sasa wamehifadhiwa katika ghala la kilichokuwa kiwanda cha mazulia Kilosa.

Baadhi ya Mitaa ya Mji wa Kilosa bado imezingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na mali za wananchi na kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment