Amnesty yatoa wito wa ukaguzi zaidi wa silaha Somalia!

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, linataka shughuli ya kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia na silaha isimamishwe.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema kuwa silaha zinazopelekewa serikali ya mpito ya Somalia, mara nyingi hutumika dhidi ya raia. Aidha, Amnesty International imesema kuwa mara nyingine silaha hizo badala ya kutumiwa na serikali huangukia mikono ya makundi yanayopinga serikali.
Nchi ya Somalia imewekewa vikwanzo vya kuingiza silaha nchini humo. Lakini, shirika la Umoja wa Mataifa lilitoaidhini kwa serikali hiyo ya mpito ambayo inakabiliana na wanamgambo wa kiislamu kupewa silaha.
Nchi ya Somalia imejaa silaha na kuna makundi mengi yamejihima kupigania mamlaka.
Lakini wakati jamii ya kimataifa inajaribu kuisaidia serikali hiyo hafifu ya Somalia, silaha zaidi zinaingizwa nchini humo.
Mwaka uliopita serikali ya Marekani ilipeleka tani 19 ya silaha Somalia.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment