Uongozi wa timu ya Africa Lyon ya jijini Dar es salaam umesema uko katika kikao kizito jioni hii na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ili kumaliza tatizo la wachezaji wa timu hiyo Castor Mumbala na Yahya Issa waliokuwa wameachwa na timu hiyo katika dirisha dogo la usajiri uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Afisa habari wa timu hiyo Kambi Mbwana amesema mpaka jioni hii viongozi wa timu hiyo na TFF wako kwenye kikao cha kujadili suala hilo na watamalizana na wachezaji hao jioni hii ili waendelee kulipwa mshahara wao na timu hiyo mpaka mkataba wao utakapomalizika.
TFF ilikuwa imewazuia wachezaji watatu wapya waliosajiriwa na Africa Lyon kucheza kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambao ni golikipa Ivo Mapunda kutoka Saint George ya Ethiopia, Meshack Abel na Adam Kingwande kutoka klabu ya simba ya jijini Dar es salaam, kutokana na mkanganyiko wa taratibu za usajiri uliojitokeza kwa wachezaji Castor Mumbala na Yahya Issa.
Kambi amesema timu hiyo imeamua kuwarejesha kundini wachezaji hao ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vyema katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo timu hiyo inatarajia kucheza na mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga, mchezo utakaochezwa jumapili kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, Africa Lyon inatarajia kwatumia wachezaji wake wapya ili kuimarisha kikosi chake na kukiwezesha kuanza vizuri ligi hiyo katika mzunguko wa pili na wa lala salama.
0 comments:
Post a Comment