RAIS JAKAYA AKUBALI KUONGOZA KAMPENI YA "MARALIA HAIKUBALIKI TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA"

Aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Mark Green akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza"
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa katikati akisikiliza jambo wakati aliyerkuwa Balozi Marekani nchini Mark Green alipokuwa akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Maralia kwenye Hoteli ya Movenpick leo, kulia ni Peter Peter Chernin (Mwenekiti wa Malaria no More Marekani ) ambaye ameungana na Balozi Mark Green katika kampeni hiyo na kulia ni Naibu waziri wa Afya Aisha Kigoda.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetangaza kuwa leo mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete amekubali kuongoza kampeni ya Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza .Leo Wizara imeungana na wasanii mashuhuri wa Tanzania, washirika wa kimataifa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara na vitengo vya sanaa kulitangazia Taifa tamasha la zinduka hapo tarehe 13 februari katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam. Tamasha hili ni kwajili ya kuwahamasisha watanzania katika kupambana na malaria.
Mwaka huu, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanikisha zoezi la utumiaji wa chandarua ya mbu na kutolewa kwa gharama nafuu kwa raia wake. Katika kuhamasisha juhudi hizi, Raisi kikwete na Malaria haikubaliki inahamasisha kila mtanzania kuwa na jukumu la kujilinda mwenyewe na familia yake katika kuidhibiti malaria.
Tanzania, kama kiongozi wa kupambana na malaria ulimwenguni, inahamasisha sekta zote za kijamii zikiwamo sekta za sanaa, biashara, na michezo kujumuika pamoja kupambana na malaria nchi nzima.
Chini ya uongozi wa Raisi na wizara ya afya na ustawi wa jamii kampeni hii ya uhamasishaji imelenga kila jamii ya kitanzania ili kubadili mtazamo wa watanzania juu gonjwa hili la malaria. Matokeo ya juhudi hizi ni kuongeza ujuzi zaidi wa kujikinga na malaria kama kulala ndani ya chandarua kilichowekwa dawa, tambua na itibu malaria mapema na hakikisha unajali na kuangalia afya ya mama mjamzito.
“Waafrika wengi hudhani malaria haiepukiki, na kwamba hakuna wanachoweza kufanya katika kuzuia gonjwa hili. Tunakwenda kuwahakikishia kuwa sio sahihi. Tunaweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria” alisema Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa “pamoja na mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete ninaamini kila Mtanzania atajiunga pamoja kutamka kuwa malaria haikubaliki nchini kwetu 2010.
Katika shughuli za mwaka 2010, Raisi Kikwete ataongoza tamasha la kitaifa liitwalo zinduka litakalowashirikisha wasanii mashuhuri wa Tanzania akiwamo msemaji mkuu wa tamasha hili lady Jay dee, Professor Jay, Tanzania House of Talent (THT na wengine wengi. kupitia vituo vya luninga na redio ujumbe wa tamasha hili utaweza kuwafikia mamilioni ya watanzani na ujumbe mahususi wa kutambua jukumu lao katika kujikinga na ugonjwa wa malaria. kwa kuongezea wasanii mahiri wa Tanzania wametunga wimbo unaozungumzia athari za ugonjwa wa malaria, wimbo uliowashirikisha wasanii 18, ushirikino mkubwa wa wasanii ambao haujawahi kufanywa hapa Tanzania.Wimbo huo umetambulishwa kwa waandishi wa habari na utaimbwa siku ya tamasha la zinduka
Ulimwengu wa muziki unanafasi kubwa katika kufikisha ujumbe kwa watanzania katika kupambana na malaria na kupata mafanikio makubwa katika kupambana na ugonjwa huu, alisema lady jay dee kama msemaji wa kampeni hii “katika tamasha la zinduka watanzania wote wataweza kupaza sauti zao kwa njia ya wimbo kwa nia moja ya kusitisha malaria nchini.
katika kuisaidia tanzania kupambana na malaria Malaria Haikubaliki itajumuisha shughuli za ushirikiano za kijamii, PSAs, ujumbe kwa njia ya luninga na radio,mabango,ngazi ya jamii,kiutamaduni, matukio ya kimichezo na maonyesho ya barabarani ili kuhakikisha ujumbe wa malaria haikubaliki unaufikia kila familia nchini Tanzania. kampeni hii ya kitaifa itakuwa kwenye engo zote za ngazi ya kijamii na kila nyumba kwa kuhamasisha shughuli za kijamii zitakazotolewa na Population Services International ,Johns Hopkins University na shughuli za district advocacy zitakazoongozwa kwa sauti moja.kwa wakati huo chama cha msalaba mwekundu Tanzania kitakuwa pamoja na katika kampeni za nchi nzima
Kutoka kwenye jamii ya imani Malaria Haikubaliki imehusisha baraza la kiristo nchini na baraza la kiislam kuwahusisha viongozi wa kiimani na waumini wao kuweka juhudi katika kupambana na malaria nchi nzima
Barani Africa malaria haiathiri maisha ya watu tu bali jamii nzima, malaria inasababisha mtu mmoja kukosa kazini kwa siku kumi na tano ndani ya mwaka na familia inatumia zaidi asilimia 25 ya kipato cha familia katika kutibu malaria barani Africa. Malaria ni kikwazo katika maendeleo, inakadiriwa barani Afrika dola bilioni 12 kila mwaka zinapotea na asilimia 40 zinatumika katika masuala ya afya.katika kupambana na ugonjwa huu, Tanzania imeweza kuonyesha jinsi Africa peke yake inavyoweza kujikwamua kutoka kwenye mzigo wa malaria na kuendeleza mikakati yake ndani na nje ya mipaka.
Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza inaongozwa na serikali ya Tanzania na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Washirika wengine katika kampeni hii ya kupinga malaria ni Roll Back Malaria Partnership, Malaria No More, Population Services International, Johns Hopkins University Center for Communication Programs, Tanzanian Red Cross, United Against Malaria, MEDA na World Vision with support from the Global Fund.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment