Makamu wa Rais atoa Msaada wa Baiskeli!!

=Katibu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Elisha Suleiman akimwelekeza jinsi ya kuendesha baiskeli ya miguu mitatu mlemavu wa viungo Rufiya Juma Khamis (15) wa Chokocho,Pemba muda mfupi baada ya kumkabidhi baiskeli hiyo ili iweze kumsaidia kuanza shule kutokana na kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umbali kati ya nyumbani na shuleni. Wanaoshuhudia ni Wazazi wake Bwana Juma Khamis Idd na Bi Naima Bahari Juma. Baiskeli hiyo imetolewa msaada na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk Ali Mohamed Shein.
Picha/Clarence Nanyaro…VPO

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Bora Unaetoa baiskeli kuliko wanaotoa DINNER la mchana kwa wachezaji.Tunajifanya kama BONGO tuko safi kumbe siyo kivile kabisa.

Post a Comment