DIAMOND MUSICA YAMCHOMOA MULEMULE KUTOKA FM ACADEMIA

Mkurugenzi msaidizi wa bendi ya Diamond Musica Perfect Kagisa katikati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati uongozi wa bendi hiyo ulipotangaza wanamuziki wake wapya watano waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni.
Perfect amesema wamemchukua mmoja wa wanamuziki nguli wa bendi pinzani ya FM Academia Mulemule au FBI ambaye atakuwa kiongozi wa bendi hiyo kwa sasa huku wakiwatwaa wanamuziki wengine wanne kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao ni Kabongo Mamale, Sone Masamba, Guy Bonheur, Pirro Jazzo na Patien Losso ambaye anapiga gitaa la sollo.
Amesema wamedhamiria kufanya mambo makubwa kwa mwaka huu wa 2010 na ndiyo maana wameanza na kasi ya kuongeza wanamuziki ili kuimarisha kikosi chao cha uimbaji na unenguaji pia kwa upande wa wanaume "lakini pia tukaona tuimarishe upande wa gitaa la sollo kwa kumchukua huyu Patien Losso".
Amesema bendi hiyo inatarajia kuingia kambini januari 26 wiki ijayo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya nyimbo mpya na kuunganisha wanenguaji katika kucheza staili mbalimbali zilizobuniwa kabla bendi hiyo haijaanza rasmi kufanya mambo yake ikiwa na wanamuziki wake wapya, wengine waliopo katika picha waliokaa kutoka kulia ni Kabongo Mamalee mwanamuziki, Juddy Moshi Mkurugezi wa bendi hiyo na kushoto ni Mulemule kiongozi wa bendi hiyo na Alan Mulumba kashama aliyeko mwisho.
Wanamuziki wa bendi hiyo wakionyesha vitu vyao mbele ya wanahabari mara baada ya mkutano.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment