Kikosi cha timu ya Simba
Kikosi cha Mtibwa Sugar
Kikosi cha Mtibwa Sugar
Baada ya watani wao wa jadi Yanga ya jijini Dar es salaam kuishindilia Mafunzo ya Zanzibar magoli 6-0 jana na kutinga Nusu Fainali kwenye uwanja wa uhuru katika michuano ya kombe la Tusker, Simba nayo imezinduka na kuisambaratisha Mtibwa Sugar ya Munungu Morogoro magoli 2-1 kwenye uwanja huohuo wakati wa mchezo mwingine wa Kombe la Tusker.
Ilikuwa ni timu ya mtibwa Sugar iliyokuwa ya kwanza kufunga goli kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia kwa mchezaji wake Said Mkopi katika dakika ya 42 baada ya kupachika goli safi na kuichanganya ngome ya simba, goli lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Katika kipindi cha pili Simba ilizinduka na kutafuta magoli ya ushindi kwa nguvu jambo ambalo lilizaa matunda baada ya mchezaji wake Mussa Hassan Mgosi kuifungia timu hiyo goli la kwanza, goli hilo liliongeza kasi ya mchezo wa timu ya Simba na kumfanya mchezaji wake Haruna Moshi Boban akishirikiana vyema na wenzake kuongeza goli la pili kwenye mchezo huo.
Mpaka mwisho wa Mtanange huo Simba imetoka uwanjani na ushindi wa 2-1 dhidi ya mtibwa Sugar na kutokana na ushindi huo sasa Simba imefikisha pointi 4 na kuingia moja kwa moja kwenye nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la Tusker.
0 comments:
Post a Comment