Miss East Africa kucheza na Jide na Banana!

WASHIRIKI wa shindano la Miss East Africa leo wanatarajiwa kushuhudia onyesho la wanamuziki Lady Jaydee na Banana Zoro.
Jide akiwa na bendi yake ya Machozi leo watatumbuiza kwenye ukumbi wa Zhong Hua Victoria wakati Banana atakuwa Thai Village Masaki.
Akizungumza jana, Msemaji wa Miss East Africa, Petter Mwendapole alisema washiriki hao wametaja kuwafahamu wasanii hao wawili hivyo wakaona ni vyema wakahudhuria maonyesho yao.
“Watakuwa Zhong Hua kwa Jide lakini baadaye watakwenda mara moja tu kwa Banana lakini rasmi kwa Banana watakuwepo Jumapili Cine Club,” alisema.
Mwendapole alisema wiki ijayo warembo hao watafanya shughuli za kijamii.
Shindano la Miss East Africa litafanyika Ijumaa Ijayo kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa sh 100,000 ambapo watakaolipa watapewa na chakula na tiketi za kawaida sh 50,000.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment