Kikwete aongoza Watanzania kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru uwanja wa Uhuru!

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya uhuru yaliyofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo asubuhi.
(picha na Freddy Maro)
Amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua majeshi ya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Uhuru yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika uwanja wa taifa kusherehekea miaka 48 ya uhuru.
-Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru katika uwanja wa taifa leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment