KIINGILIO cha juu katika shindano la Miss East Africa kitakuwa sh 100,000 !

KIINGILIO cha juu katika shindano la Miss East Africa kitakuwa sh 100,000 ambapo watakaolipa pia watapewa na chakula cha jioni.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, msemaji wa Miss East Africa, Petter Mwendapole alisema katika shindano hilo litakalofanyika Desemba 19 kwenye ukumbi wa Mlimani City, kiingilio cha chini kitakuwa sh 50,000.“Kiingilio cha laki moja kitakuwa kwenda na chakula ambacho kitatolewa na kampuni ya Ako Catering Service,” alisema.
Alisema tiketi kwa ajili ya shindano hilo litakaloshirikisha nchi 10 zitaanza kuuzwa leo sehemu mbalimbali mjini Dar es Salaam.
Baadhi ya sehemu ambazo tiketi hizo zitapatikana ni pamoja na Tina Maria Boutique, Engen Mbezi, Engen Ubungo, Engen Mbezi, Samaki Samaki Mlimani City, TCC Club Chang’ombe, Steers, Best Bite Namanga, Shear Illusion.Tayari warembo kutoka Mauritius, Kenya, Djibouti, Somalia,Rwanda wameshawasili na wako kambini hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.Miss East Africa inaandaliwa na Rena Events na kudhaminiwa na CMC Automobile, Kings and Queens Worldwide, New Habari (2006) Limited, East Africa Radio na Televisheni, DD Whole Sale.
Warembo wakipata chakula cha mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment