FULLSHANGWE IKAJIMUVUZISHA MPAKA MASHUJAA VINGUNGUTI, HEBU PATA MAMBO MDAU!!

wanamuziki wa bendi ya Vibration Sound Elistone Angai akiwaongoza wanamuziki wenzake wa Bendi hiyo wakati wa onyesho lao walilofanya jana wakati wa kusherehekea miaka 48 ya uhuru wa Tanzania kwenye ukumbi wa Mashujaa uliopo Vingunguti jijini Dar es salaam.
Elistone ameongeza kuwa kwa sasa wako mbioni kuingia Studio ili kurekodi nyimbo zao tatu ambazo tayari wamezitunga na zimekamilika kwa asilimia 100%, Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Safari yenye vikwazo iliyotungwa na Jadu Fieldforce, Salamu ya bure iliyotungwa na Germa Kisa, na Moshi wa sigara iliyotungwa na Patent Budar ambapo jina la albam hiyo litakuwa Safari yenye Vikwazo.
Mwanamuziki huyo mkali kwa kupiga gitaa la Sollo ameongeza kuwa wanafikiria kufanya kazi na maproducer wawili ambao ni Omary Mkali na Malon Linje hii inatokana na uwezo wao katika kutengeneza muziki hasa wa dansi
Amemaliza kwa kusema muziki ni kazi nzuri ambayo yeye kama mwanamuziki anaiheshimu na kujituma kwa bidii ili kuendesha mambo yake ya kimaisha na ndiyo maana mpaka leo yumo kwenye gemu na anaendelea vyema "unajuaa wanamuziki wengi hawako Serious kabisa kwenye muziki wamekuwa wakibebwa tu na vyombo vya habari kwa sababu hawajui matatizo ya kuwabeba, muziki ni kama Bondia huwezi kumbeba kwenye vyombo vya habari kwani siku ya mwisho yeye ndiye atakayepanda ulingoni na atajitetea na kutoa jasho ikibidi damu yeye mwenyewe na mungu wake vivyo hivyo na kwa mwanamuziki utabebwa kwenye magazeti lakini jukwaani utapanda mwenyewe bila vyombo vya habari anamaliza Elistone.
Mirinda Nyeusi ambaye ni rapa wa bendi ya Vibration Sound akiwa katika picha ya pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment