Mama Salma Kikwete akiwa amemshika mtoto.
Na Anna Nkinda - Maelezo, aliyekuwa Ruvuma
08/11/2009 Jumla ya Tshs. 112,080,000/= zinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa zahanati ya Lusoga iliyopo wilayani Mbinga katika mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa wakati akikabidhi ripoti ya wilaya ya Mbinga kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa wa Ruvuma.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwezi wa tisa mwaka huu hadi sasa wananchi wameshiriki kuleta matofali ya kuchoma 70,000, mawe tripu 60 na uchotaji wa maji kwa ajili shughuli za ujenzi hivyo kufanya nguvu za wananchi kufikia Tshs. 5,800,000/=.
"Halmashauri kwa upande wake inakusudia kugharamia uwekaji wa umeme, maji pamoja na uzio wa zahanati kazi itakayogharimu Tshs. 30,000,000/= pia wahisani kutoka Jamhuri ya watu wa Korea kupitia shirika la Medical Peace Foundation wametoa mchango wa Tshs. 82,080,000/= na hadi sasa wametoa kiasi cha Tshs. 24,730,413.02", alisema Kanali Mstaafu Mjengwa
Aliendelea kusema kuwa lengo kuu la ujenzi wa zahanati hiyo ni kupunguza msongamano katika Hospitali ya wilaya kwa kuweza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi kwani ujenzi wa zahanati hiyo ukikamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 7,000.

0 comments:
Post a Comment