MAISHA CLUB ILIVYOTEKETEA KWA MOTO LEO MCHANA!!

Kama linavyoonekana jengo ilimokuwemo Maisha Club lilkiwa limeungua na kuteketea kabisa kutokana na moto ambao unadaiwa kuanza kuwaka mida ya saa saba mchana hata hivyo imeelezwa kuwa vikosi vya kuzima moto vilichelewa kufika katikaeneo la tukio na kukuta moto huo umesambaa eneo kubwa na kuunguza sehemu kubwa ya club hiyo na kuunguza karibu vifaa vingi vilivyokuwa vikitumika katika club hiyo hali ndiyo kama hivyo wadau tunampa piole mama yetu Hellen Swea na msimamizi wake Dj Majay kwa kupatwa na matatizo hayo mungu awape nguvu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu kwako.
Vyombo vya muziki vikiokolewa kutoka katika club hiyo na wafanyakazi wa vikosi vya kuzima moto hata hivyo moto huo umeteketeza mali nyingi ambazo mpaka sasa thamani yake bado haijafahamika.

Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima moto wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio kwani karibu jengo zima la club hiyo limeungua.

Moto ukiteketeza majengo a club hiyo ya usiku leo mchana vifaa vingi vimungua kwa moto na kuteketea.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment