Rais Kikwete aifariji Familia ya Marehemu Ng'itu Mbezi Beach!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa Ruangwa CCM marehemu Sigfrid Ng'itu wakati Rais Kikwete alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mbezi beach Dar es Salaam kuifariji familia yake.Marehemu Ng'itu alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu Septemba 15 mwaka huu akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Prisca Ng'itu mke wa Marehemu Sigfrid Ng'itu aliyekuwa Mbunge wa CCM Ruangwa wakati Rais Kikwete alipokwenda kuifariji familia ya Marehem huko mbezi beach,jijini Dar es Salaam jana jioni.(picha na Freddy Maro)


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment