Aliyekuwa mwanamuziki wa bendi kadhaa za muziki nchini ikiwemo TOT,DoubleM Sound na nyinginezo Rashid Mwenzingo wikiendi hii aliwasilimia kisaniiwanamuziki wa bendi ya K-mondo sound waliokuwa wakitumbuiza katika ukumbiwa Triz Motel uliopo Mbezi jijini Dar es salaam.Mwenzingo aliingia ukumbini hapo kwa lengo la kuangalia shoo hiyo kamawashabiki wengine wa K-mondo lakini alijikuta anapanda jukwaani baada yakukunwa na moja ya vibao vilivyopigwa na bendi hiyo ambavyo vinginealiwahi kuviimba katika bendi alizowahi kufanyia kazi.Mwenzingo ambae kwa sasa anaimba katika bendi ya Msondo alipanda jukwaanihapo na kuimba sambamba wana Kmondo kama ishara ya salam kwa wasaniiwenzake wa bendi hiyo.“Kama ilivyo kawaida yetu wasanii huwa tunasalimiana kisanii”alisema.Bendi ya K-mondo ambayo hufanya maonyesho katika ukumbi huo wa Triz uliopoMbezi kila siku ya Ijumaa inaongozwa na Richard Mangustino sambamba nawanamuziki wengine akiwemo Vumi, Toto Tundu ‘ Panduka’ na wengineo.
Mwenzingo atumbuiza K-mondo
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment