Giraffe watia mkono ziara ya Ferre Gola!!

Mwanamuziki Ferre Gola

Timu ya Ferre ikiwajibika jukwaani.

Hoteli ya Giraffe Ocean View ya jijini Dar es salaam imejitokeza kudhaminiziara ya mwanamuziki kutoka Kongo Ferre Gola.Akizunguza meneja mkuu wa hotel hiyo mjini Dar es salaam, Nayak S.K. Rahulalisema “Tumejitolea kudhamini ziara ya Ferre Gola kutoka Kongo ambapojukumu la malazi pamoja na chakula kwa yeye pamoja na wanamuziki wakeitakuwa juu yetu”.Alisema kuwa mwanamuziki huyo mahiri ataweka makazi yake katika hotelihiyo kwa siku zote ambazo atakuwepo mjini Dar es salaam.
Giraffe wamekuwa miongoni mwa wadhamini wa mwanzo kabisa wa ziara hiyoambayo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaamkwa mwaliko wa kampuni ya New Habari (2006) ikushirikiana na NYProduction.
Mbali na ziara hii hotel ya Giraffe pia imekuwa ikidhamini ziara namaonesho mbali mbali nchini ikiwemo Miss Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment