Bia ya Kilimanjaro yamzindua DC Same!!

Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahimu Marwa (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa mwanariaadha, Francis Naali kabla ya kuanza kwa mbio maalumu za kukimbia mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi kilele cha mlima kilimanjaro.Mbio zenye ujumbe wa “Fikisha Tanzani katika hatua ya juu zaidi” na kudhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro.

Mwanariadhaa, Francis Naali akianza mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi katika kilele cha mlima kilimanjaro. Mbio hizo zilianza jana wilayani same huku zikiwa na ujumbewa "Fikisha Tanzania katika hatua ya juu zaidi" zimedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro.

Na Mwandishi Wetu, Same

MAPOKEZI makubwa ya wanariadha wanaokimbiza bendera ya Taifa kwenda kilele cha Mlima Kilimanjaro, yamemzindua Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahim Marwa na sasa ameahidi kuelekeza nguvu zake katika kukuza mchezo huo wilayani mwake.
Marwa aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa anakabidhi bendera ya Taifa kwa mwanariadha nyota Francis Naali, aliyeanzisha ngwe ya mwisho ya mbio hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Naali alikuwa anaanzisha mbio kumalizia kilomita 104 kati ya 567 walizokimbia wanariadha zaidi ya 70 tangu kuanza kwa mbio hizo Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam na kuendelea kwa siku nne mfululizo, zikipita katika mikoa ya Pwani, Tanga na hatimaye Kilimanjaro.
“Jamani, nimehamasika sana na ninawashukuru Bia ya Kilimanjaro kwa kuipa Same heshima ya kuwa na kituo cha mbio hizi. Binafsi nimehamasika na ninatangaza rasmi kwamba, kuanzia sasa nitaweka mkazo katika riadha wilayani kwangu.
wakiianza ngwe ya mwisho ya mbio hizo.
Naye Meneja Masoko wa TBL, David Minja akiwa mwenye tabasamu, alisema: “Tunajivunia kampeni hii ya kupandisha bendera katika Mlima Kilimanjaro, na kikubwa tunashukuru kwa jinsi Watanzania walivyopokea kampeni hii ya “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”. Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu ya Kilimanjaro…”
Kauli ya shukrani kwa wakazi wa mikoa waliyopitia wanariadha hao ilitolewa pia na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Alisema; “Leo ni siku ya nne ya mbio hizi za aina yake na tunashukuru kwa mwamko ambao Watanzania wameuonyesha kote tulikopita.Sisi wa Bia ya Kilimanjaro tuko kamili na tunajipanga kuhakikisha mbio hizi zinapata mafanikio zaidi na zaidi, lengo likiwa kwenda sambamba na umaarufu wa mlima wa Kilimanjaro.”
Bia hiyo, ndiyo inayozidhamini klabu kongwe na maarufu zaidi katika soka nchini, Simba na Yanga, pia ni mdhamini wa muda mrefu wa mbio za kimataifa za Marathoni za Kilimanjaro na zile zinazoshirikisha wanariadha kutoka zaidi ya nchi 25 duniani.
Pia ni wadhamini wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro. Imekuwa pia ikidhamini michuano ya mpira wa kikapu ya mkoani Dar es Salaam `RBA Kili’.
Mbio hizo zilitarajiwa kuingia Marangu jana jioni, tayari kwa kuipandisha kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment