VODACOM YAZINDUA PROMOSHENI YA ‘ONGEZA SALIO KWA M-PESA NA UJISHINDIE SIMU YA BURE’

Vodacom Tanzania leo imezindua promosheni mpya ijulikanayo kama ‘ONGEZA SALIO KUPITIA M-PESA NA UJISHINDIE SIMU YA BURE’ kwa wateja wake wote wa Malipo ya Kabla na VodaJaza. Sasa wateja waliojisajili na M-PESA wanaweza kuongeza muda wa maongezi kwenye simu zao au za marafiki zao kwa M-PESA na wabahatike kujishindia simu aina ya Motorola W230. Droo zitachezeshwa kila Jumatatu kuwapata washindi 10 watakaojinyakulia simu ya Motorola W230 KILA MMOJA. Vilevile, wateja watapata nyongeza ya asilimia 5 BURE kila waongezapo salio kwa M-PESA. Mfano: Ukiongeza Tsh 2,000 kwa M-PESA utapata Tsh 100 ZAIDI BURE!

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment