Na Anna Nkinda - Maelezo, Morogoro
20/10/2009 Serikali imetumia jumla ya shilingi milioni 105 kujenga na kufanya ukarabati wa majengo mbalimbali katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kilakala iliyopo mjini Morogoro.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa shule hiyo Paulina Mkwama wakati akisoma taarifa ya shule kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea shuleni hapo.
Mwalimu Mkwama alitoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo kuwa shilingi milioni 70 zimetumika kukarabati mabweni, shilingi milioni 13 zimejenga nyumba ya walimu moja yenye uwezo wa kuishi familia mbili na shilingi milioni 22 zimejenga bweni jipya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 48.
Shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa gari la shule, ongezeko la wanafunzi wahitaji ambao ni yatima na wanaotoka katika familia duni kwani licha ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kuwasomesha wanafunzi watano pia kuna wanafunzi 40 ambao hawana ufadhili.
"Kutokukamilika kwa ujenzi wa uzio wa shule kunaathiri sana usalama na ulinzi wa wanajumuia wa shule hii na mali zao, kutokukamilika kwa nyumba ya walimu, bweni na maabara ya elimu ya viumbe hai, uchakavu wa majengo upungufu wa vitanda 48 vya bweni jipya na makabati 24 pia ni tatizo katika shule hii", alisema.
Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa "Incinerator" kwa ajili ya kuchomea taka ngumu pia mabweni hayana vifaa vya kisasa vya kujihadhari na majanga ya moto.
Akiongea na wanafunzi wa shule hiyo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii huku wakiwatii walimu wao na kujiepusha na vitendo vitakavyowapelekea kupata mimba na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Mama Kikwete alisema, "Elimu ndio msingi wa maendeleo ya mwanadamu unaomwezesha kujinufaisha na mazingira yake naungana na wengi walioandika juu ya umuhimu wa elimu kama silaha muhimu na endelevu dhidi ya maradhi na umaskini".

0 comments:
Post a Comment